Kwa mashabiki wa klabu ya Simba inaweza kuwa neema baada ya mchezaji wao kipenzi Emanuel Anold Okwi kutua Dar hapo jana.
Okwi aliwasili jijini kwa ndege na kupokewa na makamu wa rais wa klabu ya Simba Geoffrey Nyange 'Kaburu' katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere.
Strika huyo amekuja rasmi kumwaga wino kwa ajili ya kuimarisha kikosi cha Simba ambacho kitashiriki kimataifa baada kutwaa kombe la FA.
Okwi ataungana na nyota mwingine wa zamani wa klabu ya Simba Shomari Kapombe ambaye amerejea kwa mara nyingine akitokea Azam FC.
Picha na Simba App.
Picha na Simba App.

Comments
Post a Comment