Timu ya AS Roma imewatolea nje Liverpool iliyoweka mezani ofa ya £28 milioni kwa ajili ya usajili wa Mohamed Salah.
Hata hivyo chanzo cha habari kupitia Sky Italy kimeripoti kuwa bado mazugumzo baina ya timu hizo mbili yanaendelea.
Salah mwenye miaka 24, aliwahi kuitumika Chelsea baada ya kusajiliwa kwa dau la £11 milioni akitokea FC Basel ya Uswis na baadae aliuzwa kwenda Roma kwa dau la £15 milioni.
Mshambuliaji huyo thamani yake imepaa baada ya kuifungia Roma mabao 15 katika ligi ya Serie A msimu uliopita.

Comments
Post a Comment