Salah amwaga wino Liverpool.


Aliyekuwa mshambuaji wa AS Roma Mohamed Salah amesaini miaka 5 Liverpool kwa dau la paundi 34.3 milioni.

Raia huyo wa Misri aliwasili jana katika uwanja wa Melwood ambapo alifanyiwa vipimo na kusaini mkataba na Liverpool.

Salah anakuwa mchezaji wa pili wa kusajiliwa na Liverpool baada ya usajili wa mshambuliaji kinda Dominic Solanke ambaye aliachwa na Chelsea baada ya kumaliza mkataba wake.

Salah amekabidhiwa Jezi namba 11 na mshambuliaji Roberto Firmino amekabidhiwa jezi namba 9 ambayo iliachwa na Christian Benteke.

Comments