Mshambuliaji wa AS Roma ya Italy Mohamed Salah huenda akasaini Liverpool muda wowote kuanzia sasa.
Mazungumzo baina ya Liverpool na AS Roma yanaendelea vizuri na huenda mchezaji akatua Anfield baada ya kufikia makubaliano ya paundi milioni 35 kama ada ya uhamisho.
Raia huyo wa Misri angetua Liverpool mwaka 2015 lakini aliyekuwa kocha wa Chelsea Jose wakati huo Mourinho aliwazidi ujanja vijogoo hao wa Merseyside na kumnasa nyota huyo kutoka FC Basel kwa dau la paundi milioni 12.

Comments
Post a Comment