Nahodha wa Taifa Stars Mbwana Ally Samatta hakupendezwa na matokeo ya sare katika mchezo wa jana dhidi Lesotho ambapo matokeo yalikuwa 1-1.
Samatta alizungumzia hisia zake baada ya kupigwa swali na waandishi habari baada ya kuonekana alikasirikia mchezo huo.
"Sipendezwi na matokeo ya sare wala kushindwa, tulikuwa nyumbani hivyo tulitakiwa kushinda na kupata pointi tatu muhimu."
Mbali na Lesotho pia kikosi hicho cha Salum Mayanga bana wana kibarua kizito cha kukabilia na Uganda pamoja na Cape Verde kuelekea kufuzu fainali za mataifa Afrika nchini Cameroon.

Comments
Post a Comment