Schneiderlain ajiachia na wamasai Ngorongoro.


Kiungo wa Everton Morgan Schneiderlain ameonekana akiwa mwenye furaha katika maeneo ya Ngorongoro mkoani Arusha pamoja na jamii ya wamasai.

Kiungo huyo bado anamalizia fungate baada ya hivi karibuni kufunga ndoa na aliyekuwa mpenzi wake wa siku nyingi.

Nyota huyo wa Everton aliposti baadhi ya picha akionekana mwenye furaha na amani pamoja na mkewe wakicheza kwa pamoja na watoto wa kimasai na kuchukua picha mbali mbali  za kumbukumbu.

Comments