Taifa Stars imeanza na ushindi COSAFA.


Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars ' imeanza vizuri kwenye michuano ya COSAFA nchini South Africa baada ya kuichapa Malawi mabao 2-0.

Mabao hayo yaliwekwa nyavuni na winga wa klabu ya Simba Shiza Kichuya ambaye alifunga mabao hayo ndani ya dakika nzuri.

Ushindi huo ni hatua nzuri kwa kocha wa timu ya Taifa Salum Mayanga ambae ana kibarua kigumu cha kuandaa kikosi imara ili kupigania nafasi ya Kufuzu michuano ya kombe la FA nchin Cameroon.

Comments