Simba yasalimu amri kwa Nukuru All Stars.


Timu ya Simba imechemka kusonga kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la Sportpesa baada ya kung'olewa na Nakuru All Stars kutoka Kenya.

Mchezo huo uliamuliwa na matokeo ya penati baada ya timu hizo kutoshana nguvu ndani ya wa dakika 90 uwanjani ambapo Simba ilichemsha baada ya Daniel Agyei kupaisha mkwaju wa penati.

Nakuru All Stars ambayo inashiriki ligi daraja la kwanza kutoka Kenya itakutana na Gor Mahia ambayo ni ya Kenya pia na Yanga itachuana na FC Leopards kutika nusu fainali.

Comments