Mshambualiaji wa Yanga Amis Tambwe hajafahamu hatma yake ndani ya klabu hiyo licha ya mkataba wake kuelekea ukingoni.
Mpaka sasa uongozi wa Yanga haujasema chochote kuhusiana na mpango wa kuendelea na huduma ya Strika huyo.
Tambwe alisema kuwa ataondoka na kutafuta maisha maisha sehemu nyingine endapo timu itaendelea kuwa kimya hadi Julai mwaka huu.
"Kama waajili wangu watakuwa kimya, nitatafuta maisha sehemu zipo zipo timu hapa ndani zinahitaji huduma yangu na hata nje ya nchi hii maisha yanatafutwa." Alisema Tambwe.
Tambwe ameifungia Yanga mabao 46, Tangu alipojiunga na timu hiyo akitokea Simba SC.

Comments
Post a Comment