Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa amesema hayupo kwenye mipango ya kocha Antonio Conte kwenye kikosi cha timu hiyo.
Costa aliyasema hayo baada ya mchezo wa kimataifa wa Hispania dhidi ya Colombia ambao ulimalizika kwa sare ya bao 2-2.
"Nilishafanya maamuzi na mashabiki walijua kuwa sitaondoka Chelsea msimu ujao.
"Ni aibu, pamoja na kuweka wazi maamuzi yangu kuhusu Chelsea msimu ujao lakini Conte alinitumia ujumbe kwenye simu kwamba sipo kwenye mipango yake msimu ujao."
Costa mwenye miaka 28 aliifungia Chelsea bao 20 katika mechi 35 alizoichezea timu hiyo kwenye ligi ya EPL kwa msimu uliomalizika.

Comments
Post a Comment