USAJILI: Gnabry atua Bayern Munich


Aliyewahi kuwa winga wa Arsenal Serge Gnabry amejiunga na Bayern Munich baada ya kusaini mkataba wa miaka 3.

Gnabry mwenye miaka 21 aliondoka Arsenal mwaka 2012 na kutua West Brom kwa mkopo ambapo msimu uliopita alijiunga na Werder Bremen ya Ujermani.

Gnabry alikuwa kwenye kiwango bora msimu uliopita baada ya kutupia bao 11 katika mechi 27 alizocheza na kuivutia Beyern Munich.

"Ni heshima kubwa kwangu kujiunga na timu kubwa na bora kama hii." Alisema Gnabry.

Comments