Vicent Bossou bado yupo njiapanda.


Beki wa Yanga Vincent Bossou amesema kuwa bado hajafanya maamuzi iwapo ataendelea kubaki na Mabingwa hao au kutafuta maisha sehemu nyingine.

Kulingana na chanzo cha gazeti la Champion bado nyota huyo hajafahamu  hatma yake katika klabu ya Yanga licha ya kuhusishwa kwenye usajili wa Singida United.

"Sifahamu lolote kuhusiana na mustakabali wangu ndani Yanga, sijafanya mazungumzo na viongozi wa timu hiyo tangu nilipomaliza mkataba wangu.

" Nipo mapumzikoni nyumbani, nasubiri waniite nifanye nao mazungumzo kama wanahitaji huduma Yangu." Alisema Bossou.

Comments