Liverpool walivyochomoa kugeuzwa kitega uchumi katika soka.


Hivi karibuni timu ya Liverpool ilionesha kuvutiwa na beki wa kiholanzi Virgil  van Djik ambaye anafanya vizuri kwa sasa tangu alipotua Southampton akitokea Celtic.

Virgil alisajiliwa kwa dau la £11 mwaka 2015 na kuonesha uwezo mkubwa, akiwa na msimu mmoja ameweza kuzishawishi baadhi ya timu kubwa ikiwemo Liverpool na Manchester city.

Hivi karibuni Liverpool iliripotiwa kuwepo kwenye mchakato wa kumsajili Virgil vam Djik kutoka Southampton ambayo kwa siku za hivi karibuni imekuwa ikiwafaidisha Liverpool wachezaji akiwemo Adam Lallan, Nathaniel Clyne, Dejan Lovren na Sadio Mane.

Licha ya kiwango kizuri na kutambulika kwa uwezo wa Sadio lakini £32 milioni pekee ndizo zilimng'oa Mane na kumfanya atue Anfield ambapo amefanya vizuri baada ya kuifungia mabao 13 msimu uliomalizika licha ya majeruhi yaliyokuwa yakimuandama.

Liverpool ambayo iliwaaminisha Southampton katika usajili wa Virgil van Djik imewataka radhi viongozi wa timu hiyo baada ya kughairi kuendelea na mazungumzo ya kumsajili Djik.

Bila shaka dau ambalo Southampton wamelipanga kwa ajili ya mchezaji huyo liliwastua Liverpool licha ya beki kuonesha wazi wazi kuichagua Liverpool nje ya klabu zingine ambazo pia zimekuwa zikimtolea macho.

Bosi wa Liverpool Jurgen Klopp anajua wazi anahitaji kiongozi aliye timamu katika safu ya ulinzi wake ambayo imekuwa ikiwaangusha mara kadhaa katika baadhi ya michezo kwenye ligi kuu lakini amebadili uamuzi na kuendelea kuangaza huku na uko huenda akabahatika kupata beki bora kwei ambayo inaeleweka.

Van Djik ni mchezaji mzuri ambaye ni wazi kama atatua Liverpool, huenda akapunguza shida ya ulinzi kutokana na kuwa imara katika kucheza mipira ya juu na chini lakini dau lake limekuwa kikwazo.

Southampton wanamweka sokoni beki huyo kwa £70 milioni ni pesa nyingi ambayo unaweza kusajili nyota wakali na maarufu duniani kama kina Gareth Bale na Antonio Griezmann.

Klopp anaona wazi hiyo ni biashara isikuwa na uwiano na iliyokosa usawa na kuwapelekea Liverpool kuwaomba radhi Southampton ambao tayari waliweka wazi kwenye umma kuwa wameshaanza mazungumzo na Liverpool.

Hakuna anayebisha kwamba soka la sasa ni biashara, pamoja na hayo lakini Van Djik hafikii thamani ya paundi milioni 70 ukilonganisha na ubora alionao.

Virgil van Djik anapoteza ndoto zake za kutua Liverpool kutokana na mfumo wa sasa ulipo katika soka la Ulaya, ambao umetanguliza zaidi maslahi na kuwafanya wachezaji kuwa mtaji mkubwa katika ngazi ya usajili na si kama ilivyokuwa katika nyakati za nyuma.

Ubora wa Christiano Ronaldo ndiyo ulioishaiwishi Man Utd kumwachia nyota huyo kwa dau nono la paundi milioni 80 na ni wazi alistahili kulinganishwa na ubora wake na tayari alikuwa amefanya mambo makubwa.

Thamani ya van Djik hailingani na paundi milion 70. Binafsi nawaunga mkono Liverpool kwa kuokoa kiasi hicho cha pesa ambacho huenda wakitulia wanaweza kusajili wachezaji wazuri na wenye vipaji kama ilivyokuwa kwa Sadio Mane na Mohammed Salah ambaye waamfukuzia kwa sasa.

Ni jana tu Chelsea imekataa kutoa dau la paundi milioni 70 kumsajili James Rodriquez ambaye amepoteza namba ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Zinedine Zidane katika kikosi cha Real Madrid.

Haingii akilini mchezaji aliyesajiliwa kwa dau la £50 kutoka Monaco, na kwa sasa hana namba ya kudumu kikosini umpige bei kwa paundi milioni 70, ni wazi hapo hakuna uwiano katika biashara ya soka.

Bado Liverpool ina nafasi ya kuvuna wachezaji wazuri na wenye vipaji kwa dau hilo Van Djik. Nawapa hongera kwa kuwa wamekataa kugeuzwa mtaji kwa mchezaji ambaye huna uhakika kama atadumu katika kiwango hicho siku zote.

Comments