Mwenyekiti wa kamati ya usajili Simba SC Zacharia Hanspoppe amesema kuwa mlango upo wazi kwa mchezaji anayetaka kuondoka.
Hanspoppe alisema wamechoshwa na wimbo wa taarifa za kuondoka kwa baadhi ya wachezaji wa Simba akiwemo Jonas mkude, Abdi Banda na Ibrahim Ajib.
"Tulikubaliana nao kulingana na vile walivyohitaji, lakini leo unasikia kesho vile, kama yupo mchezaji anayetaka kuondoka Simba basi ruksa." Alisema Hanspoppe.
Jonas Mkude na Ibrahim Ajib wanahusishwa na mpango wa kuhamia Singida United au Yanga na Abdi Banda anafukizia dili lake South Africa.

Comments
Post a Comment