Wanyama wa Spurs aja kula bata Tanzania.


Baada ya David Beckham na Mamadou Sakho kufanya utalii nchini Tanzania Hatimaye kiungo wa Tottenham Victor Wanyama ametua Tanzania.

Wanyama anakuwa nyota wa pili kutoka Spurs kuja kutalii Tanzania mwaka huu zikiwa zimepita siku mbili tangu alipotua nyota mwenzake kutoka Spurs Christian Eriksen.

Wanyama ambaye ni raia wa Kenya amezitaja timu za Simba na Yanga kuwa ndizo anazozifahamu.

Comments