Waziri: Mashabiki wa Azam subirieni raha.


Mshambuliaji mpya wa Azam Waziri Junior amewatoa hofu mashabiki wa Azan FC baada ya kuwaambia watarajie raha uwanjani.

Hayo yalisemwa jana na mshambuliaji huyo alipokuwa akitambulishwa rasmi na msemaji wa timu hiyo Jaffar Iddi baada ya kupewa nafasi kuzungumza.

"Napenda kuishukuru Toto Africans, uongozi na wachezaji wao kiujumla kwa ushirikiano wao walionionesha hadi natua Azam.

" Nategema ushirikiano huo pia katika timu, naahidi kuwa sitawaangusha na mashabiki watarajie mambo mazuri kutoka kwangu." Alisema Waziri.

Pia mchezaji huyo alisema kuwa Azam FC ni moja kati ya timu ambazo alikuwa akiziota kuzichezea na hivyo ndoto yake imetimia.

Comments