Uongozi wa klabu ya Yanga umetangaza rasmi kuachana na kiungo wa timu hiyo Haruna Niyonzima baada ya kushindwa kufikia makubaliano.
Yanga imeshindwa kufikia kiwango ambacho Niyonzima amekuwa akihitaji ili asaini mkataba mpya wa kuitumikia timu hiyo kwa miaka miwili mbele.
Mabingwa hao wa ligi kuu Tanzania Bara wamemtakia Kiungo kila la kheri baada ya kudumu ndani ya klabu hiyo kwa misimu sita.

Comments
Post a Comment