Beki wa zamani wa Barcelona Dani Alves ameitosa Manchester city na kusaini kwa wababe wa Ufaransa Paris Saint Germain.
Alves mwenye miaka 34 alivunja mkataba wake na Juventus kwa madai ya kujiunga na kocha wake wa zamjani katika timu ya Barcelona Pep.
Raia huyo wa Brazil bado anaonekana mwenye kiwango kilicho bora licha ya umri kumtupa mkono kwa sasa.
Alves aliweza kuisaidia Juventus kutwaa ubingwa wa Serie A na kuingia katika fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya ambayo walipoteza mbele ya Real Madrid.

Comments
Post a Comment