Kiungo wa Ufaransa Tiemoue Bakayoko amesaini miaka 5 ya kuitumikia Chelsea kwa dau la pauni 40 milioni.
Huo umekuwa usajili wa pili ghali uliofanywa na Chelsea tangu kufunguliwa kwa kwa dirisha hilo kwenye kpindi hiki cha majira ya joto baada ya kusajiliwa Antonio Rudiger kutoka Roma.
Kwa kipindi cha wiki mbili mfululizo Bakayoko amekuwa akihusishwa kutua Stamford Bridge na hatimaye ametua.
Bakayoko 22, ameungana na kiungo mwenzake kutoka Ufaransa N'golo Kante ambaye ana msimu mmoja Chelsea.

Comments
Post a Comment