Banda apata timu South Africa.


Beki aliyemaliza mkataba na Simba Abdi Banda amekamilisha mpango wake wa kujiunga na Boroka FC inayoshiriki ligi kuu South Africa.

Banda amemaliza muda wake Simba baada ya kuiwezesha timu hiyo kupata ubingwa wa kombe la FA msimu uliopita.

Meneja wa mchezaji huyo Abdul Bosnia amesema kuwa kila kitu kipo tayari na muda wowote kuanzia sasa Banda atakuwa mchezaji wa Boroka FC.

"Kila kitu kimekwenda sawa anachotakiwa kufanya ni kujituma ingawa Boroko FC ni moja ya timu za kawaida lkn juhudi zake zinaweza kuinyanyua timu hiyo." Alisema Abdul.

Comments