Caballero wa city asaini Chelsea.


Aliyekuwa golikipa wa Manchester city Willy Caballero amesaini Chelsea kwa uhamisho huru.

Caballero mwenye miaka 35 aliachwa kwenye kikosi cha Manchester city baada ya kumaliza mkataba wake mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu.

Raia huyo wa Argentina ndiye aliyeipa Manchester city ubingwa wa taji la Capital One mwaka 2016 na baada ya kupangua penati 3.

"Nina furaha sana kujiunga na Chelsea hawa ndiyo mabingwa wa ligi kuu." Alisema Caballero.

"Nitajituma na kujitoa kwa nguvu zote na kuisaidia Chelsea kufanya vizuri katika mashindano." Aliongeza golikipa huyo.

Comments