Chelsea yakubali dili la Bakayoko.


Timu ya Chelsea imekubali kulipa dau la pauni 40 milioni kama ada ya uhamisho wa kiungo Tiemoue  Bakayoko.

Tayari Chelsea ilifanya usajili pili baada ya kumnasa beki wa Ujermani Antonio Rudiger siku chache zilizopita kwa dau la pauni 34 milioni.

Ujio wa Bakayoko unaweza kufungua njia kwa kiungo Nemanja Matic kutimka Manchester United kutoka na shaka ya namba.

Hata hivyo Chelsea inaweza isimuachie Matic kutua United kutoka na kuvuruga dili la Romelu Lukaku ambaye ameungana na Mourinho kwa mara nyingine.

Comments