CHICHARITO: Ametua West Ham Utd.


Timu ya West Ham imekamilisha usajili wa mshambuliaji Javier Hernandez maarufu kama 'Chichirito' ambaye amesaini miaka 3 akitokea Bayer Leverkusen kwa ada ya uhamisho wa £16 milioni.

Hernandez mwenye miaka 29 alitua jana jijini London na kukamilisha zoezi la vipimo kabla ya kusaini mkataba.

Raia huyo wa Mexico ndiye mchezaji anayelipwa zaidi kuwahi kutokea katika timu ya West Ham, atapokea kiasi cha £ 140000 kwa wiki.

Comments