Giroud kumrithi Lukaku Everton.


Timu ya Everton inajiandaa kuweka mezani dau la pauni milioni 90 kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Oliver Giroud.

Romelu Lukaku anakaribia kujiunga na Man Utd kwa ada ya uhamisho inayokadiriwa kufikia pauni 90 milioni.

Kocha wa Everton Ronald Koeman anataka kuziba pengo la mchezaji huyo kwa kumsajili Oliver Giroud ambaye nafasi imeanza kuwa mashakani kutokana na ujio wa Alexandre Lacazatte.

Mbali na Oliver Giroud pia kocha huyo yupo kwenye mipango ya kumleta Wayne Rooney ili kujiunga na timu yake ya zamani.

Comments