Hii ndiyo ndoto ya Ibrahim Ajib Yanga.


Mshambuliaji mpya wa klabu ya Yanga Ibrahim Ajib Migomba amesema kuwa ndoto zake ni kuweka rekodi kwa mabingwa hao wa VPL.

Ajib alisema tangu aliposajiliwa na Yanga amekuwa na ndoto za kuweka rekodi mpya katika historia ya klabu hiyo.

"Kila mmoja ana ndoto, na ndoto zangu ni kufanya mambo makubwa na kuweka rekodi mpya ndani ya klabu hii." Alisema Ajib.

Mshambuliaji huyo aliamua kuachana na Simba baada ya kumalizika kwa mkataba wake mwishoni mwa mwezi Juni.

Source: Goal.com

Comments