Himid, Mahundi warejea mazoezini Azam


Timu ya Azam imeendelea na mazoezi katika uwanja wa Chamanzi ambapo jana nyota waliokuwa katika kikosi cha Taifa Stars waliungana na wenzao kwenye mazoezi.

Wachezaji hao ni Himid Mao, Stamili Hoza na Joseph maundi ambao walikuwepo kwenye kampeni ya kusaka tiketi ya kufuza kombe la mataifa Africa (CAN) kwa wachezaji wa ndani.

Nyota hao walikosa ziara iliyofanywa na kikosi cha Azam katika mkoa wa Iringa ikiwemo mechi za kujipima nguvu dhidi ya Njombe Mji na Lipuli FC.

Comments