Mchambuzi wa masuala ya soka katika kituo cha Sky sports na Gary Neville amesema kuwa ana imani timu itakayosajili vizuri ina nafasi ya kuwa bingwa msimu ujao.
Mchezaji ambaye ni mchezaji wa zamani wa Manchester United amesema kuwa karata yake kwa kwa sasa ipo kwa mahasimu wa jiji la Manchester ambayo mpaka sasa wako mbele usajili.
Neville ana imani timu itakayosajili zaidi inayo nafasi ya kuongeza nguvu katika mashindano kutokana na uwepo wa wachezaji wengi wenye ujuzi na vipaji.
"Kila mwaka nimekuwa nikisema kuwa timu itakayosajili wachezaji wazuri na wenye vipaji huwa inabeba ubingwa, tuliona usajili wa N'golo Kante ulivyopeleka ubingwa Chelsea."
Neville anasema kuwa mambo makubwa sana yanatarajiwa kutokea katika timu hizo mbili ambazo zinaonekana kusajili wachezaji wenye vipaji.
"Sikuwa sawa kutabiri kwamba United atakuwa bingwa msimu uliopita, lakini kwa sasa naweza kusema kuwa nipo sawa." Amesema Neville.
Neville ameongeza kuwa mambo hayatakuwa rahisi kwa Mourinho ategemee changamoto nyingi kwenye mbio za ubingwa ikiwa ni pamoja na kuimarisha zaidi kikosi chake.
"Nadhani anatakiwa kutengeneza kikosi imara kuna changamoto nyingi sana kikosini hakuna urahisi katika ligi yenye kama Uingereza." Aliongeza Neville.
Manchester United imefanya usajili wa wachezaji kadhaa akiwemo Romelu Lukaku na Victor Lindelof pia wapo kwenye mipango ya kumsajili Ivan Perisic kutoka Intermilan.
Kwa Upande wa City mpaka sasa wamesaji wachezaji wanne akiwemo Erderson, Bernardo Silva, Kyle Walker na Douglas Luis kutoka Brazil.

Comments
Post a Comment