Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Yanga Hamis Kiiza amewatonya Yanga kuhusiana na usajili wa kiungo Tony Maweje.
Kiiza amewataka Yanga kumsajili mchezaji huyo kwani watakuwa wamelamba dume kutokana uwezo mkubwa alionao.
Maweje amekuwa aking'ara na kikosi cha taifa cha timu ya Uganda kutokana na uwezo wake mkubwa wa kukaba na kupiga mashuti.
Zipo taarifa kuwa kiungo huyo yupo tayari kutua nchini kwa ajili ya kuitumikia Yanga ambayo kwa muda imekuwa ikisaka kiungo bora wa kukaba.
Maweje mwenye miaka 30 amewahi pia kucheza soka kulipwa katika nchi ya Sweden katika timu ya Hausegund.

Comments
Post a Comment