Liverpool yazuia usajili wa Sturridge.


Soko la usajili limezidi kuwa gumu katika bara la Ulaya hali inayopelekea mastaa kadhaa kuzuiwa kuondoka kwenye klabu zao akiwemo Daniel Sturridge wa Liverpool.

Sturridge mwenye miaka 27 anawindwa na timu ya West Ham pamoja na PSG na tayari West Ham ilianza mikakati hiyo tangu mwishoni mwa Ligi.

Klopp amezuia usajili wa nyota huyo akiwa na hofu huenda wakawa na wakati mgumu wa kupata mtu sahihi atayeziba pengo la Sturridge.

Mambo yamezidi kuwa magumu kwenye soko la usajili  kutokana na msimamo uliopo kwenye kila timu ambayo italazimika kutumia gharama kubwa katika usajili.

Comments