Man City imefanya usajili mwingine leo.


Aliyekuwa beki wa Tottenham Kyle Walker amesaini Manchester city kwa ada ya uhamisho wa pauni milioni 50.

Walker mwenye miaka 27 anaingia kwenye orodha ya mabeki ghali zaidi duniani akiwemo David Luis na John Stones.

Kocha wa timu hiyo Pep Gurdiola aliwaacha mabeki wote wa pembeni ambao walimaliza mkataba wao akiwemo Gael Clichy, Bacary Sagna na Pablo Zabaleta.

Comments