Klabu ya Manchester United imekubali kulipa kiasi cha Pauni 75 milioni ili kumnasa Romelu Lukaku kutoka Everton.
Aliyekuwa mshambuliaji wa timu hiyo Zlatan Ibrahimovic ameshindwa kuendelea na Man Utd kwa msimu mwingine na hivyo Mourinho ameamua kuigeukia Everton.
Lukaku mwenye miaka 25 aligoma kuongeza mkataba mpya ikiwa ni dalili ya kutaka kutimka Goodson Park.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka Sky Sports kimeeleza kuwa mashetani hao wekundu hawana kipingamizi juu ya dau hilo.

Comments
Post a Comment