Milioni 100 zamwondoa Bossou Yanga.


Yanga imeamua kuachana rasmi na aliyekuwa beki wa timu hiyo Vincent Bossou ambaye amedai milioni 100 za usajili.

Baada ya mazungumzo klabu ya Yanga imeshindwa kufikia mwafaka na raia huyo wa Togo anayedai kiasi hicho cha pesa ili kusaini mkataba mpya.

Uongozi wa Yanga umetangaza kuachana na mchezaji huyo baada ya kushindwana kwenye dau la usajili kama ilivyokuwa kwa aliyewahi kuwa kiungo wa timu hiyo Haruna Niyonzim.

Comments