Mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara Yanga SC wako mbioni kumsajili beki wa kati kutoka Nigeria Henry Tony Okho.
Usajili huo utakuwa wa mwisho kwa mabingwa hao ambao wamemalizana na Papy Kabamba hivi karibuni.
Yanga imeweka kambi yake katika mkoa wa Morogoro ambapo wamekuwa na mazoezi makali ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu pamoja na mchezo wa Ngao ya hisani dhidi ya wapinzani wao Simba.

Comments
Post a Comment