Msamaha wa TFF wanaukia kwa Manara.


Kamati ya nidhamu ya TFF ambayo iliundwa hivi karibuni huenda ikaawachia huru msemaji wa Simba Haji Manara na wakala wa wachezaji Damas Ndumbalo.

Ndumbalo na Manara wote kwa pamoja walifungiwa kwenye kutojihusisha na masuala ya soka katika uongozi wa Rais Jamal Malinzi.

Kamati hiyo imebaini kuwa Manara na Ndumbalo walifungiwa kutokana na kile kinachoitwa 'Figisu'

"Nadhani kuna tatizo baada ya kupitia tena, hata Jerry Muro anayemalizia kifungo anaonekana kufungiwa kimakosa" kilieza Chanzo kutoka TFF

Comments