Msuva aipa Yanga mkono wa kwa heri


Winga mwenye kasi Tanzania Simon Msuva hatakuwepo katika kikosi cha Yanga msimu ujao.

Kiungo huyo anaondoka leo nchini kuelekea Morocco na kijiunga na klabu yake mpya ya Difaa El Jadida.

Msuva anaeleka Rabbati Morocco ambapo atakamilisha zoezi la vipimo na kusaini mkataba.

Nyota huyo wa Tanzania ataungana na Ramadhani Singano 'Messi' ambaye naye amesaini mkataba na timu hiyo.

Comments