Kiungo wa Taifa Stars Mzamiru Yasin amewaacha midomo wazi maskauti wanaosaka wachezaji kutokana na kiwango anachokionesha.
Mzamiru yupo South Africa kwenye michuano ya COSAFA akiitumikia Taifa Stars ambayo imetinga nusu fainali baada ya kumchomoa mwenyeji kwenye hatua ya robo fainali.
Kiungo huyo wa Simba amekuwa injini ya Taifa Stars kwenye eneo la kiungo ambapo uwezo wake mkubwa wa kuliendesha gurudumu la kikosi hicho umekuwa gumzo kuzivutia baadhi ya timu.
Moja ya magazeti katika nchi hiyo yametoa ripoti kuwa mchezaji huyo anafatiliwa kwa karibu sana na timu ya Bidvest pamoja Mpumalanga Black Ace ameripoti Saleh
Jembe kupitia blog yake.
Mchezaji huyo huenda akabaki nchini humo endapo atapokea dili la kujiunga na moja kati ya timu zilizovutiwa na uwezo wake.

Comments
Post a Comment