Nahodha wa Ndanda ametua Singida Utd.


Aliyekuwa nahodha wa timu ya Ndanda FC ya Mtwara Kigi Makasi amesaini mkataba kuitumikia Singida United.

Kigi amekuwa mchezaji wa mwisho kufunga usajili wa klabu hiyo kwa mwaka 2017/18 ambacho kinanolewa na Mholanzi Hans Pluijm.

Pia mchezaji huyo amewahi kuitumikia Klabu ya Yanga ambao ni mabingwa wa ligi kuu mara tatu mfululizo.

Comments