Neymar aimaliaza Man Utd US Tour.


Mshambuliaji fundi wa Barcelona Neymar ameifungia timu hiyo bao pekee la ushindi dhidi ya Manchester United katika uwanja wa Maryland nchini Marekani.

Neymar alifunga bao hilo kipindi cha kwanza katika dakika ya 31 ya mchezo huo baada ya Antonio Valencia kufanya uzembe.

Bao hilo lilidumu hadi mwisho wa mchezo na kuifanya Manchester United kupoteza mechi ya kwanza baada ya kushinda dhidi ya LA Galaxy, Salt Lake, Man city na Real Madrid.

Comments