NYONI: Usajili mwingine Yanga SC.


Beki wa Taifa Stars Erasto Nyoni huenda akajiunga na klabu Yanga baada ya kufanya mazungumzo na klabu hiyo.

Nyoni 29, amemaliza mkataba na klabu ya Azam na sasa ni mchezaji huru ambaye anaingia kwenye orodha ya nyota kadhaa ambao wameondoka Azam.

Hivi karibuni vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti mpango wa Yanga kumsajili Erasto Nyoni.

Nyoni ni moja kati ya wachezaji wachache ambao ambao wana uwezo wa kuchezaji nafasi tofauti uwanjani hasa katika eneo la ulinzi na kiungo.

Comments