Omog: Mayanja ndiye kiboko ya Yanga.


Kocha wa Simba Joseph Omog amesema kuwa hawezi kuruhusu Mayanja kuondolewa Simba kwa kuwa anaijua vema dawa ya Yanga.

Hivi karibuni kumekuwa na taarifa kuwa Simba ilitaka kuachana na kocha huyo na kuajiri kocha mwingine ambaye ni raia wa Kirundi.

Hata hivyo Omog ambaye hivi karibuni alirejea nchini baada ya likizo amesema kuwa bado anataka kufanya kazi na Mayanja ambaye ni raia wa Uganda.

"Mayanja anaijua Yanga, bado nataka kufanya kazi na yeye, anaifahamu vizuri Yanga kuliko mimi." Alisema Omog.

Comments