Rasta amesaini Yanga miaka 2.


Kiungo mkabaji kutoka Congo Papy Kabamba Tshishimbi amesaini mkataba wa miaka 2 katika klabu ya Yanga.

Rasta amesaini mkataba huo leo baada ya kufuzu zoezi la vipimo ambalo lilifanyika jana.

Mchezaji huyo alikuwa ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa wanaunda kikosi cha Mbabane Swallos ya Swaziland ambayo iliichomoa Azam FC kwenye michuano ya kombe la Shirikisho.

Comments