Rooney ajipanga kurudi alipotokea.


Mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney yupo kwenye mipango ya kujiunga na timu ya Everton ndani ya wikiendi ya wiki hii.

Rooney mwenye miaka 31 alitokea Everton FC kabla ya kutua Manchester United mwaka 2004.

Everton ambayo kwa sasa inaonekana kujipanga vema kwenye usajili inajipanga kumrejesha nyota huyo ili kuongeza nguvu kwenye kikosi chao.

Raia huyo wa England aliwahi kuitumikia Everton kwa kipindi cha misimu miwili tangu mwaka 2002 hadi mwaka 2004.

Wayne Rooney amepoteza namba kwenye kikosi cha kwanza cha kocha wa sasa wa Manchester United Jose Mourinho.

Comments