Uongozi wa Simba umetangaza rasmi kuachana na aliyekuwa kocha msaidizi wa timu hiyo Jackson Mayanja.
Mayanja alisema kuwa amepokea taarifa kwa viongozi wa Simba kwamba hatakuwa sehemu ya benchi la ufundi wa timu hiyo.
"Nilijua kuwa siku moja sitakuwa sehemu ya Simba pengine kwa hiari yangu au kwa mtizamo wa Viongozi wake." Alisema Mayanja.
Raia huyo wa Uganda amewahi kufundisha kikosi cha kagera Sugar miaka 3 iliyopita kabla ya kujiunga na Simba SC.

Comments
Post a Comment