Kiungo mshambuliaji wa Manchester City Kevin De Bruyne amesema kuwa haitashangaza endapo timu hiyo itanyakua taji la ligi kuu England.
De Bruyne ana imani kuwa jitihada zinazofanywa na kocha wa timu hiyo Pep Gurdiola ikiwemo usajili wa nyota wapya utazaa matunda.
"Hakuna kazi rahisi kwenye vita ya ubingwa, kuna timu 6 nazo zinawania ubingwa.
"Jitihada za kocha wetu zinaonekana, ni mwanzo mzuri, haitashangaza tukifanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu." Alisema De Bruyne
Raia huyo wa Ubelgiji yupo na kikosi cha Manchester city ambacho kiweka kambi kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu.

Comments
Post a Comment