Sajili 3 kubwa barani Ulaya leo.


Manchester City huenda ikawaweka rekodi mpya duniani na ndani ya klabu hiyo endapo itatoa kiasi cha £143 milioni kumsajii mshambuliaji wa Monaco Kylian Lottin Mbappe kama ilivyoazimia.

Liverpool inaonekana kuridhia kumpiga bei kiungo wake mjermani Emre Can baada ya Juventus kuweka mezani dau la £30milioni kama ada uhamisho wa mchezaji huyo. Pia mchezaji huyo amemaliza kufanya makubaliano binafsi na Juventus.

Barcelona imepeleka ofa nyingine ya kiasi cha £80 milioni katika timu ya Liverpool ili kumsajili Phelipe Coutinho. Tayari zipo taarifa kuwa Coutinho amekubaliana mambo binafsi na Barcelona.

Comments