Mashabiki wa klabu ya Yanga wamejawa na furaha kubwa baada ya kurejea kwa mshambuliaji Donald Ngoma na kumwaga wino ndani ya timu hiyo.
Kulikuwa na presha kubwa kwa mashabiki wa Yanga baada ya kuvuma kwa taarifa mbali mbali ambazo zilikuwa zikimuhusisha mchezaji huyo kutua Simba.
Hata hivyo Ngoma amekata mzizi wa Fitina baada ya kusaini kuitumikia Yanga kwa miaka miwili mbele.
Mashabiki wa Yanga wana imani kubwa kuwa timu hiyo itandelea kufanya vizuri mbele ya mpinzani wao Simba baada ya kufanikisha kuwalinda baadhi ya wachezaji.

Comments
Post a Comment