Aliyewahi kuwa mshambuliaji wa Manchester United Javier Hernandez atajiunga na West Ham baada ya kukamilisha zoezi la vipimo hapo kesho.
Hernandez mwenye miaka 29 atakuwa ndiye mchezaji anayelipwa zaidi kuwahi kutokea katika klabu ya West Ham ambapo atapokea kiasi cha £140000 kwa wiki.
Tayari mazungumzo kati ya Bayer Leverkusen na West Ham United yamekwenda vizuri na Hernandez maarufu kama 'Chicharito' atarejea tena England.
Raia hiyo wa Mexico aliwahi kuitumikia Manchester United tangu mwaka 2010 hadi na 2015 na kuifungia mabao 59 katika mechi 156 alizowahi kuichezea timu hiyo.

Comments
Post a Comment