Mshambuliaji wa Everton Romelu Lukaku amebaki njiapanda kwenye zoezi la usajili wake kutokana na kuwaniwa na timu mbili tofauti.
Hadi kufikia jana zipo taarifa kuwa Chelsea imefikia dau la pauni milioni 75 ili kufanikisha usajili wa Romelu Lukaku.
Wakala wa mchezaji huyo Mino Raiola anataka kufanikisha usajili wa mchezaji huyo kwa upande wa timu ya Manchester United.
Uhusiano kati ya kocha wa Chelsea Antonio Conte na uongozi wa timu unaweza kuingia kwenye mgogoro endapo Lukaku atafanikiwa kutua Man Utd.
Kumekuwa na taarifa kuwa Conte ameshindwa kutimiziwa katika kile kinachodaiwa ni orodha ya wachezaji anaowahitaji, Chelsea haijaonesha dalili ya kutoa fedha kufanikisha usajili huo.
Lukaku mwenye miaka 24 maono yake ni tofauti na wakala wake huyo ambaye ni raia wa Italy akitamani zaidi kutua Chelsea kuliko Man Utd.
Bado Lukaku atakuwa amebaki njiapanda endapo Chelsea watazubaa kuchangamkia dili hilo ni rahisi kwa wakala Mino Raiola kumpiga bei Man United.
Hadi kufikia jana timu ya madaktari ikitokea Man Utd ilitua Los Angels (LA) ili kufanikisha zoezi la vipimo kwa mchezaji huyo.
Lukaku ameonekana akifanya mazoezi katika na swahiba wake Paul Pogba huko Los Angels Marekani siku ya jana.

Comments
Post a Comment