Yaliyojiri jioni hii kwenye usajili barani Ulaya.


Manchester city imekubali kulipa dau la paundi 50 milioni ili kukamilisha usajili Kyle Walker kutoka Tottenham Hotspurs.

Gurdiola amewaacha mabeki watatu wa pembeni akiwemo Gael Clichy, Bacary Sagna na Pablo Zabaleta ambao wote kwa pamoja walimaliza mkataba wao.

Awali mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy alisema kuwa hawatamuachia beki huyo chini ya dau la Pauni 50 milioni.

Baada ya kufikia makubaliano hayo, Walker mwenye miaka 27 ataingia kwenye zoezi la vipimo muda wowote kuanzia sasa.

Comments