Timu ya Liverpool imeamua kurudi na ofa ya pili ya £70 milioni ili kama ada ya uhamisho wa kiungo Nabi Keita kutoka RB Leipzing ambayo ilichomoa ofa ya kwanza.
Manchester United itamtoa kati ya Chris Smalling au Matteo Darmian ili kuishawishi Intermilan kumwachia Ivan Perisic.
Everton imeandaa kiasi cha £30 milioni kumsajili winga Theo Walcott kutoka Arsenal.
Mshambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge amekataa kujiunga na moja ya timu za China ambayo ilitaka kumsajili nyota huyo wa England.
Stoke city wameitaka West Ham kutoa kiasi cha £22.5 milioni ili wamwachie mshambuliaji wao Marko Arnautonovic.
Man Utd inataka kumtua golikipa wao David De Gea kama sehemu ya kufanikisha usajili wa kiungo Tony Kroos kutoka Real Madrid.
Tottenhma inajipanga kukamilisha usajili wa kiungo Rose Barkley kutoka Everton kabla ya kuanza safari yao kuelekea Marekani.
Leicester imeitaka AS Roma kutoka Italy kutoa kiasi cha £40 milioni kama ada uhamisho wa mchezaji Riyad Mahrez.

Comments
Post a Comment